NGAO YA HISANI...ARSENAL YAIVURUGA VILIVYO MAN CITY


Mchezaji Mikel Arteta akiibusu ngao ya hisani wakati timu yake ilipowacharaza mabingwa wa msimu uliopita wa Ligi kuu nchini Uingereza timu ya Manchester City kwa mabao 3-0 kwenye uwanja wa Wembley, Jumapili. Ngao hii huwa ni ishara ya ufunguzi wa kuanza kwa msimu mpya wa Ligi, ambapo humkutanisha bingwa wa Ligi wa msimu uliopita dhidi ya bingwa wa kombe la chama cha soka (FA)  





Wachezaji wa Arsenal wakishangilia na ngao yao...




Meneja mkuu wa timu ya Arsenal (kocha) mfaransa Arsene Wenger akikiongoza kikosi chake wakati mpambano ukiendelea...




Mshambuliaji wa kifaransa, Santi Carzola (kulia) akipiga shuti na kupachika bao la kwanza kwa Arsenal huku mlinzi Gael Clichy wa Man City akijaribu kuzuia. Anayeshuhudia kwa karibu ni Yaya Toure wa Man City




Aaron Ramsey akipachika bao jingine kwa Arsenal huku akiwa amezongwa vilivyo na mlinzi Gael Clichy wa Man City...

 

Kocha Arsenal Wenger ameuanza vema msimu. Hongera. Je, ataumalizaje! Tusubiri na tuone...

No comments: