HONGERA MWANANGU KWA KUTIMIZA MIAKA 3...


Ni binti yangu mdogo, anaitwa Sumaiyah. Anasoma shule ya awali iitwayo Nalopa iliyopo maeneo ya Njiro jijini Arusha. Mwezi huu wa 8 ndio ikawa ametimiza mwaka mwingine mpya maishani mwake. Baada ya kumfanyia dua na kumwombea heri kwa yule aliyemuumba, basi mambo mengine yakaendelea kama kawa....

...hii ni keki yake iliyozungukwa na paketi kibao za biskuti, aliyoandaliwa na bibi yake. Hata mimi niliionja; ilikuwa tamu kwelikweli

  


...akiwa amesimama kwenye keki yake akijiandaa kuikata!





...amefurahi; meno yote ya utoto nje akiwa amesimama na dada yake, dada Shadya.





...akiwa na familia yake.




...akimlisha keki baba yake.




...akimlisha keki mama yake, Khadija Abdallah Chembe, mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa jamii, Dar es Salaam .

 

 

...akimlisha keki mama yake mdogo, Faidha wa shule ya msingi Nalopa.




...akilishwa keki bibi yake, bibi Zainabu Saidi Kivuyo mtumishi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha vijijini.




...baada ya hekaheka zote, hatimaye akapumzika; akakaa chini na kuanza kupata JUISI ya matunda taratiiiiiiiibu. 

                                  Shughuli hii ilifanyikia Njiro-Tsunami.

No comments: