Kwa haraka tu, unaweza ukahisi hapa ni kwenye mbuga fulani hivi ya wanyamapori! Hapana, wakwetu. Hapa ni ndani ya Jiji la Arusha, maeneo ya Ngaramtoni ya chini; ni korongo (mto wa msimu) linaloambaa ambaa jirani kabisa na uwanja wa ndege wa Arusha na pia jirani na nyumba ya wafungwa (Gereza la Arusha.) Mpini Wa Shoka na 'wife' wake walikuwa wakielekea mahali fulani, ndipo wakajikuta wamepotea njia na kuibukia kwenye korongo hili! Hata hivyo tulinasuka na kuendelea na safari yetu. Hili eneo linafaa sana hata kwa kuigizia filamu fulani hivi tamu sana. Au wewe unaonaje?




No comments: