VITUKO DIMBANI..! Hii ingetokea pande za nchi zetu za kiafrika, basi ndio tungelisakamwa kweli.. Lakini hapa ni London; kwenye uwanja wenye ulinzi wa kila aina... wee acha tu, mwanawane...!
Hebu angalia kwa makini…! Shabiki kakurupuka mbio kutoka jukwaani; akaingia uwanjani wakati timu ya Tottenham Hotspur's ikijiandaa kupiga faulu yake kuelekea lango la timu ya West Ham United kwenye uwanja wa Upton Park, mjini London. Jamaa alifanikiwa kuipiga faulu hii japo shuti lake lilikuwa dhaifu tu na kudakwa kirahisi na mlinda mlango wa West Ham United; na baadaye alitiwa mbaroni na walinda usalama wa uwanjani. Ilikuwa katika mojawapo ya mechi za ufunguzi wa ligi kuu ya Uingereza zilizopigwa Jumamosi-16/08/2014. Tottenham Hotspur's ilishinda 1-0
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment