WATOTO WANAPOSAFIRI KWENDA MKOA MWINGINE KUMWONA MTOTO MWENZAO...
Kutoka jijini Arusha, watoto (kuanzia kushoto) Sumaiyah Jigge anayesinzia, Shadya Jigge mwenye ua mkononi, Faidha Mustafa (aliyebeba mtoto) na Saad Abdillahi, hivi karibuni walisafiri hadi ndani ya Chuo cha Polisi (C.C.P) mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwenda kumpongeza mtoto mwenzao, Mahamba Amini Mujengwa (anayecheka katikati), baada ya kupata mdogo wake mpya (aliyebebwa na Faidha). Kwa hakika, wote walifurahi sana kwa michezo mbalimbali.
Huyu ndiye mtoto mwenyewe mpya; kidume cha nguvu. Hongera sana Bw. Mahamba kwa kumpata mdogo wako. Aisee, mpende na umtunze.
No comments:
Post a Comment