Kompyuta mbele ya macho yake, na huku pembeni pakiwa na chupa, ambayo sijui kama ni tupu au ndani yake kuna maziwa ya moto! Chai ya rangi! Kahawa au chai ya maziwa! Nilimnasa na yeye akipekua pekua vitu ndani ya intaneti. Mambo ya www.mpiniwashoka.blogspot.com. Akijihisi uchovu kidogo, anajimiminia kilichomo ndani ya chupa na kulainisha koromeo, kisha anaendelea kupekua. Huyu ni Bi mkubwa mwenye umri wa miaka 79, aitwaye Fatuma Mohamed Laizer, maarufu kama mama Hassani Tilya, mkazi wa Majengo-Arusha. Mambo ya utandawazi haya!
|
No comments:
Post a Comment