Usifikiri hii ni shehena ya magunia ya mahindi, maharagwe au ya mkaa. Hapana, wakwetu! Ni mambo ya usafi wa mtaa hayo! Hizi ni taka za aina mbalimbali kutoka kwenye majumba na sehemu za biashara za wakazi wa kata ya daraja mbili Mjini Arusha. Eneo hili wamejiwekea utaratibu wa kumlipa mwenye gari hili kila mwisho wa mwezi, kwa ajili ya kukusanya taka na kuzipeleka kwenye jalala kuu, nje kidogo ya mji. Wakazi wa eneo hili hawasubiri hadi hicho kijiko kimoja cha halmashauri (kwenye picha ya juu) kimalize kazi kwanza katika majalala yote, ndipo kiwafikie wao! Ratiba ya kuchukuliwa taka hapa kwa gari hili ni kila siku ya Alhamisi, ingawa kwa dharura wakati mwingine ratiba huwa ibadilika ghafla. Na ninyi kwenye mtaa ama kata yenu, mnao utaratibu kama huu? Au kazi yenu ni kupiga makelele na kulalamika hovyo tu! KUHAKIKSHA USAFI, NI JUKUMU LAKO MWENYEWE. KAMA HUJUI, SHAURI YAKO!
|
No comments:
Post a Comment