RAHA YA BOMBA, LIWE LINATOA MAJI.


Bwana mdogo akikinga maji kwa raha zake. Kati ya moja ya huduma muhimu kuliko zote ndani ya maisha ya viumbe ndani ya dunia hii ni upatikanaji wa maji, tena maji safi na salama. Ukitaka kukiona kizaazaa cha maisha, basi ukose maji, hasa ya kunywa na kupikia, kwa muda wa wiki 1 au 2 tu hivi! Kwa hakika, utajihisi ni kama vile dunia yote imekuelemea. Kama wewe ni mmoja wa wakazi wa mtaa, kijiji, kitongoji, kata tarafa au mji wenye tabu ya huduma ya maji, kwakweli nahodha wako wa Mpini Wa Shoka ninakupa pole sana. Kama vipi, zungumza tu na huyu bwa'mdogo akufanyie maarifa, kama yeye anavyojichotea kwa ulaini tu kwenye hili bomba. MAJI NDIO HUDUMA NAMBARI WANI KWA VIUMBE NA MIMEA YOTE. 


No comments: