ARUSHA-MAMBO YA WACHINA HAYA!

Hii siyo njia ya kuingilia ndani ya mgodi wa machimbo ya madini! Wala hili siyo handaki kwa ajili ya wanajeshi kujificha wakati mapambano ya kivita! Wakwetu! Pia hili siyo daraja linajengwa kwa ajili ya magari na watu kupita! Ni vijimambo tu hivi vya kitaalamu vya ndugu zetu wazee wa HU! HA! Hapa ni eneo la Soko kuu-Arusha. Kwa miaka mingi eneo hili limekuwa na kawaida ya kufurika maji nyakati za mvua, maji ambayo huwa yanatiririka kwa wingi kutoka katika viunga vya mlima Meru, hasa kupitia maeneo ya Mianzini na Sanawari. Ni kero iliyokuwa haina mfano kwa wafanyabiashara wa soko hili kuu. Lakini sasa kero hii imepatiwa chanjo. Wachina wanaoboresha barabara za mji wa Arusha wako kazini katika eneo hili, wakijenga mfereji huu mkubwa unaopita chini kwa chini, ambao utakuwa na kazi moja tu ya kuyasomba maji yote yanayotuama katika eneo hili na kuyaunganisha kwenye mifereji mingine mikubwa, ili yasafiri bila ya bughudha wala kero kwa wananchi, hadi katika bwawa kuu la maji machafu. Safi sana.   


No comments: