NAO WANAHITAJI KUPENDWA NA KUSIKILIZWA.



Picha hizi 3 za Bi mkubwa huyu nilizinasa wakati akiimba na kucheza nyimbo moja tamu kwa lugha ya nyumbani kwao mkoani Kigoma(Kiha), nyimbo iliyohusu juu ya upendo baina ya wapenzi wawili. Katika moja ya umri ambao watu wengi tunafikiri kupendwa na kusikilizwa huwa kumekwisha, basi ni huu. Wakati mwingine utawasikia watu fulani wakimwambia mtu mwenye umri kama huu kwamba, "Aaa! Wapi, wewe! Hayo mawazo yako ni ya kizee... ni ya kizamani hayo, hayana maana... hayawezi kufaa tena chochote hapa!" Lakini mambo yakiwageukia na kuwachachukia, utawaona hao mbio, kwa sauti za juu, "..hebu kwanza twende tukapate ushauri kwa mzee nanihii, halafu ndipo tujue cha kufanya." Jamani tuwapende, tuwatunze na kuwasikiliza hawa wa umri huu. Pamoja na 'kula kwao chumvi nyingi', lakini pia wameona na kuyapitia mengi. Ohoo! Wee, Shauri yako siku na wewe 'yatakapokunukia'!  


No comments: