ARUSHA-SIYO BARABARA NA MITAA YA KATIKATI YA MJI TU PEKEE! HATA NJE YA MJI NAKO KAZI ZIMEPAMBA MOTO!

Hii siyo kambi ya vifaru vya jeshi la njano, wakwetu! Ni magari pamoja na mitambo ya Wachina ikiwa kazini. Ni ujenzi wa kuunganisha lami kwenye barabara ya Njiro kutoka eneo ilipokuwa imeishia lami (stendi ya zamani Njiro), ambayo inatarajiwa kujengwa hadi mji wa Kwa mromboo. Barabara hii itakapokamilika, mbona itakuwa ni kicheko tu kwa kwenda mbele kwa wakazi wa maeneo haya ya Njiro na kote itakakopita! Kwani, adha na karaha ya vumbi la kukata na shoka wakati wa kiangazi, pamoja na tope zito la kukwamisha magari makubwa kwa madogo wakati wa mvua, itakuwa imewakimbia. Hata nyumba nazo zitaanza kufutwa vumbi, na kupakwa rangi! 


No comments: