Hapa, usifikiri palikuwa na vita ya mawe iliyopiganwa muda mfupi tu! Hapana. Ni vijimambo tu hivi vya Wachina wakiendelea na ukarabati. Baada ya kumaliza kujaza vifusi, kushindilia na kumwagia maji ya kutosha, sasa wamepafunika na nailoni (iliyowekewa mawe kwa juu ili isipeperushwe na upepo) tayari kwa maandalizi ya kuweka lami ya mwanzo. Na wewe ukifuatana moja kwa moja na huyu jamaa unayemwona hapa, basi mwishoni mwa barabara hii, nyote mtajikuta mmetokea mbele ya lango kuu la kuingilia magari soko kuu la Arusha. Huu ni mmoja ya mitaa ambayo kwa miaka mingi ilikuwa ni mibovu kupita kiasi. Ni mtaa uliopo ubavuni mwa msikiti wa Bondeni.
|
No comments:
Post a Comment