JUMAMOSI TAREHE 22/09/2012 YALIKUWA NI MAAFALI YA 4 YA DARASA LA SABA KWA SHULE YA MSINGI NALOPA ILIYOPO KATA YA ENGUTOTO (ENEO LA NJIRO KWA MSOLA). MAMBO YALIKUWA MENGI MNO. LAKINI PAMOJA NA YOTE HAYO, PIA PALIFANYIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA MAENDELEO YA SHULE AMBAPO WASTANI WA SHILINGI ZA KITANZANIA MILIONI 13 ZILIPATIKANA. Mpini Wa Shoka UNAKUPA MAMBO YALIVYOKUWA KWA UCHACHE TU
Hawa ni walimu wa madarasa ya watoto wadogo (Babies&Nusery) wakiwa na baadhi ya wanafunzi wao. Aliyevaa shati jekundu ni mwalimu Happy Onesmo. Na mwenye fulana nyeupe ni mwalimu Jesca Urio.
Hawa ndio wanafunzi wa babies & Nusery. Wanajaribu kuwekwa sawa na kupangwa vizuri na mwanafunzi mwenzao wa darasa la juu. Unajua tena umri huu ni kazi kwelikweli!
Mwalimu Suzan Minja akiwapashapasha moto vijana kwa kuwaimbisha nyimbo kadhaa wakati mgeni Rasmi akisubiriwa kwa hamu
Bwana mkubwa Anko Saadi Abdillahi na Mdogo wake, Shadya Jigge, (aliyeshikwa bega na mwenzake), wa madarasa ya Babies&Nusery nao pia walikuwepo uwanjani tayari kumpokea mgeni Rasmi
Hapa, mgeni rasmi alikuwa amekaribia kabisa viwanjani. Mwalimu Longino Vincent Nkana na kinasa sauti mkononi, akiwa kazini katika kuwapanga na kuwaelekeza wanafunzi hapa na pale.
No comments:
Post a Comment