USISAHAU! BADO BARABARA NA MITAA YA MJI WA ARUSHA INAENDELEA KUFANYIWA KWELI NA WACHINA....

Pamoja na kwamba barabara na mitaa kadhaa imekwishakamilishwa na inapendeza vilivyo sasa kwa lami mpya, lakini bado kazi kubwa inaendelea......


Hapa ni kwenye mtaa maarufu wa Highland, jirani kabisa na stendi kuu ya mabasi. Wachina wanafanya kweli.  



Hapa ni maeneo ya Noble House (Nobo Hausi). Mtaa huu unaangaliana na mtaa wa Highland (huku anakotokea huyu jamaa). Na ukimfuata huyu jamaa huko anakoelekea, unakwenda kukutana na barabara ya Sokoine (Uhuru Road). Majengo ya rangi ya pinki ni mali ya shirika la nyumba Tanzania-N.H.C



Hapa ni nyuma ya shule ya sekondari ya Arusha (Arusha Sec). Hii ni mojawapo ya barabara mpya zilizochongwa miaka ya hivi karibuni ili kupunguza msongamano wa magari. Inaanzia kwenye mzunguko (keepleft) uliopo jirani kabisa na uwanja wa N.M.C (kwa sasa ni soko jipya la wachuuzi wadogowadogo; hatua chache tu kutoka nyuma ya huyu jamaa mwenye baiskeli). Barabara hii inakwenda kutokea nyuma ya mlima Shabaha (Themi Hill), ikipitia nyuma ya maghorofa ya polisi, na kwenda kuungana na barabara ya kuelekea Njiro, eneo la Relini. Hapa wachina na mafundi wao pamoja na makatapila wanashughulikia kwanza daraja dogo barabarani, na kuuimarisha mfereji maarufu wa maji (kama unavoonekana vema kwenye picha hapo chini), uliopo pembezoni mwa ukuta wa shule ya sekondari Arusha (Arusha Sec). Kisha, baada ya hapo ndipo barabara hii nayo waipendezeshe kwa kuichapa lami. Wachina, bhwana! Yaani ni kazi tu kwa kwenda mbele hadi kieleweke.

No comments: