ARUSHA MJINI-KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO KUJAZA NAFASI YA UDIWANI-KATA YA DARAJA MBILI ZAZIDI KUSHIKA KASI...ZAZIDI KUPAMBAMOTO....

 HAWA NI wana-CUF, nao VIWANJANI WAKIOMBA KURA....


 Jukwaani, Kaimu Mkurugenzi Mipango, Uchaguzi, Siasa na shughuli za Bunge C.U.F-Taifa, bwana Shaweji Mketto, akiwa katika moja ya harakati za kumpigia kampeni mgombea wa udiwani kupitia chama chake, bwana Zakaria Hassan Zani, ndani ya mitaa na vitongoji vya kata ya daraja mbili. Na katika moja ya mambo ambayo bwana Mketto amekuwa akiyatolea ufafanuzi wa mara kwa mara mbele ya wananchi, ni swali linaloulizwa mara nyingi kwenye mikutano kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini-Chadema kinaeneza kwa bidii propaganda kwamba Chama cha Wananchi-C.U.F ni CCM 'B', kwa sababu wameungana na CCM huko Zanzibar katika kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa. Jukwaani bwana Mketto anasema hivi "..wakati wa vuguvugu la kutaka kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar, ili kuepusha hali ya uhasama na uadui uliokuwa ukizidi kuchukua sura kubwa na mbaya zaidi kila siku kwa wananchi wa visiwa hivyo, hata kufikia hatua za mauaji wakati wa matokeo ya chaguzi mbalimbali, miongoni mwa wale walioshiriki kuongoza kampeni na kufikiwa kwa makubaliano hayo ni kiongozi mkuu wa Chadema bwana Freeman Mbowe. Lakini baada tu ya uchaguzi mkuu kufanyika, na Serikali mpya ya umoja wa kitaifa kuundwa Zanzibar kwa muungano wa CCM na CUF ambavyo ndivyo vilivyojipatia wastani mkubwa wa kura za Urais na Uwakilishi, Chadema kwa sababu wao hawakupata kura za kutosha kuwaingiza katika Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa, ndipo ghafla wakaibuka na PROPAGANDA hii ya uongo, ili kwadanganya wananchi wasiujue ukweli wa mambo... kama Chadema na wao wangepata wastani wa kura za kutosha kuwemo ndani ya Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa-Zanzibar, je leo wangeinuka majukwaani kuineza PROPAGANDA hii? Kama Chadema wanabisha juu ya uweli wa hili, sisi tunavyo vielelezo vya wazi kabisa visivyo na shaka hata kidogo juu ya unafiki wao huo mbele ya wananchi wa Tanzania."    



 

Mgombea udiwani kata ya Daraja mbili kupitia C.U.F, bwana Zakaria Hassan Zani (mwenye kofia ya bluu) akiwa makini akisikiliza yanayosemwa jukwaani, kabla hajapanda rasmi mwenyewe ili kunadiwa kwa wananchi...kwa wapiga kura.


    Meza Kuu ya wana C.U.F wakati wa harakati za kampeni







Wananchi.... Wanachama na Wapiga kura wakisikiliza kwa makini

No comments: