HOSPITALINI-MOUNT MERU ARUSHA



MUDA WA JIONI WA SIKU YA IJUMAA, Mpini Wa Shoka ULIKUWA NDANI YA VIWANJA VYA HOSPITALI KUU YA MKOA WA ARUSHA-MOUNT MERU.

 

Ama kweli, Hospitalini kila mtu na pilikapilika na harakati zake, huku na kule...!

  

Unapofika tu eneo la viwanja vya hospitali kabla ya kuingia kwenye geti kuu la kuelekea kwenye mawodi, utakutana na mabango mbalimbali ya kukuongoza kama haya.



Hapo hapo nje ya geti kuu, utakutana na eneo la mapokezi (Reception)



Ndani ya mapokezi, utapokelewa na ofisi hii. Soma mwenyewe bango hapo juu.


Maeneo kadhaa ya ndani ya hospitali; mawodi na ofisi nyingine za madaktari, manesi na wahudumu wengine. Pametulia.

 


Hili limeegeshwa tayaritayari kwa dharura yoyote ile ya kubeba mgonjwa kumkimbiza haraka popote pale, au kutoka haraka hapa lilikoegeshwa na kukimbia kwenda kumchukua mgonjwa (wagonjwa) mahali popote pale ndani ya Arusha. 






Manesi na watoa huduma, nao kila mmojawao na harakati zake; huyu anakimbia huku..! Mwingine anaelekea kule..! Ilimradi ni pilikapilika tu zisizosimama.




 Wananchi waliofika kuwaona wagonjwa wao, nao ni mpishano tu. Hawa wanaelekea wodi hii..! Na wengine wanatokea wodi ile..!




Wagonjwa waliozidiwa, nao walipatiwa huduma ya kuwapeleka walikotakiwa kupelekwa...kama ni wodini au kwa daktari.



Hapa ni nje ya wodi namba sita. Wodi maarufu kwa wakazi wa Mji wa Arusha na vitongoji vyake, kutokana na kulaza zaidi watu wenye maradhi mchanganyiko (siyo yale ya kuambukiza wala wazimu na kichaa). Watu wamejazana nje wakisubiri kupewa ruhusa na madaktari wanaowapitia wagonjwa, ili wapate fursa ya kwenda kuwapa pole pamoja na mtori wa moto wapendwa ndugu, jamaa na marafiki zao waliolazwa ndani ya wodi hii. 



No comments: