IDD MUBARAK... MINAL AYDINA...

      Ni katika kumbukumbu ya kisa maarufu kwa waumini wa dini kote duniani, kumbukumbu ya Nabii Ibrahim alipoamriwa na Mwenyeezi Mungu amchinje mwanawe. Nabii Ibrahim alipoitii amri ya Mwenyeezi Mungu na kufikia hatua ya mwisho kabisa ya kukipitisha kisu kwenye shingo ya mwanawe, Mwenyeezi Mungu akamwambia amchinje kondoo badala ya mwanawe. Waislamu kote duniani baada ya kuitimiza nguzo ya kuhiji katika Mji wa Makka, ni wajibu kwao kuchinja mnyama ili kuiadhimisha kumbukumbu hii ya kisa cha Nabii Ibrahim. Hata wale ambao wao hawakuipata fursa ya kwenda kuhiji, nao pia ni wajibu kwao kuchinja. Idd hii inajulikana zaidi kama Idd ya kuchinja.



HAYA ni makundi ya waumini wa dini ya kiislamu, waume kwa wanawake, wakitoka misikitini baada ya sala ya Idd.




 







Shughuli za kuchinja na kugawa mafungu ya kuwagawia majirani na marafiki yakitayarishwa.

 







Picha ya IDD... Pozi la nguvu. Mtoto Hussein Mohamed Dudu na dada yake Kuruthum wa mtaa wa Jamhuri (Jaluo), Arusha mjini.






Baada ya msosi mzito wa Idd, ni kupumzika kwa mtindo wa aina yake; chupa kubwa ya maji baridi iko pembeni kwa ajili ya kupoozea koromeo.

No comments: