KIVUMBI CHA SIKU YA KUPIGA KURA KIMEFIKA!

Baada ya karibu siku 30  za kampeni zilizojaa vijembe, mbwembwe, vituko na kila kitu ambacho wewe unakijua juu ya shughuli na hekaheka za uchaguzi wowote ule wa kisiasa, usiku na mchana... mtaa kwa mtaa... nyumba kwa nyumba... mtu kwa mtu... na hata kukusanya wapenzi na mashabiki wa chama kutoka maeneo mengine ya kata zingine za mji wa Arusha na mikoa ya jirani ili kujaza mikutano ya kampeni ionekane ni mikubwa kuliko ya wapinzani wao, hatimaye mwisho wa yote hayo Jumapili ya tarehe 28/10/2012 ambayo ndiyo siku ya wananchi wa kata ya Daraja Mbili, Jijini Arusha kumchagua Diwani wao imefika. Kati ya sura hizi hapa chini (CCM, NCCR, CHADEMA, CUF na TLP(picha haipo), moja kati yao ndio itakayoibuka mshindi na kutawazwa kuwa ndiye Diwani mpya wa kata ya Daraja Mbili, katika kuiziba nafasi ya aliyekuwa Diwani wa kata hii aliyefariki dunia, marehemu Bashir Msangi.

    Kazi ni kwako mpiga kura wa Kata ya Daraja Mbili.

 




No comments: