DIWANI MPYA!!

Hatimaye kata ya Daraja mbili jijini Arusha yajipatia Diwani mpya. Chama Cha Demokrasia na Maendeleo nchini Tanzania-CHADEMA ndicho kimefanikiwa kujitwalia kiti hiki cha Udiwani katika matokeo yaliyotangazwa usiku wa tarehe 28/10/2012 baada ya kufanikiwa kuvibwaga vyama vya CCM, CUF, NCCR-mageuzi na TLP.

     Na mheshimiwa mteule mpya kutoka CHADEMA aliyetangazwa mshindi na kuanza kukikalia rasmi kiti hicho cha udiwani kwa kata ya Daraja mbili ni huyu hapa:-

  



HEBU tuliza kidogo jicho lako ili Mpini Wa Shoka ukupe japo kidogo hali ya mambo ilivyokuwa hiyo siku ya Jumapili ya tarehe 28/10/2012 tangu kuanza kwa mchakato mzima wa upigaji wa kura asubuhi hadi shamrashara za siku iliyofuata-Jumatatu kwa ushindi wa wana-CHADEMA.



Wapiga kura, wake kwa waume, walijijongeza katika vituo vya kupigia kura mmoja baada ya mwingine au kwa makundi katika shule za sekondari za Felix Mrema na ile ya Daraja mbili.  

 



Kazi za kutafuta majina kwenye kuta na kwenye madaftari ya wasimamizi ikafanyika






Baada ya kuhakiki majina, foleni za kupiga kura zikachukua nafasi




Wakati wananchi wakiendelea na zoezi la upigaji kura kwenye vituo, nje ya ofisi za CHADEMA kata ya Daraja Mbili Mpini Wa Shoka ukawafuma Mheshimiwa Joshua Nasari mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi mwenye simu sikioni, na Godbless Lema aliyevuliwa na mahakama ubunge wa jimbo la Arusha wakizungumza na vyombo vya habari kwa njia ya simu katika kuhamasisha masuala kadhaa. 


Baada ya zoezi la upigaji na uhesabuji wa kura kukamilika, na CHADEMA kuibuka washindi siku ya Jumapili-28/10/2012, mapambazuko ya siku ya Jumatatu na mchana wake wote ikawa ni nderemo, vicheko na chereko tu kwa wana-CHADEMA kwenye ofisi zao za kata ya Daraja mbili zilizopo kwenye mtaa wa Jamhuri. 

Makundi ya wananchi; Wakina mama ni vidole juu na wengine midomoni wakiwa na ice cream wakipoza makoo wakimsubiri kwa hamu Diwani mpya awasili kwenye ofisi za chama.

 

 HATIMAYE diwani mteule akawasili...



Mheshimiwa Prosper Remmy Msoffe akisalimiana na wananchi waliokuwa wakimpongeza kwa ushindi.


KISHA kazi ya maandamano ikaanza...

"Nasema hivi, naomba tuelewane. Haya ni maandamano kwa ajili ya kusherehekea ushindi wetu katika kata hii. Kwa hivyo, nawaomba wananchi wote tutaanzia maandamano yetu kutokea hapa ofisini, tutapita hivi.... na kisha tutatokea vile....." Godbless Lema akitoa utaratibu.




Wananchi wakaanza kujipanga tayari kwa maandamano

 


Maandamano ya kusherehekea ushindi yakachukua nafasi. Yakafikia tamati kwa kuhitimishwa kwa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya mwisho wa lami-Sinoni. Hapa mambo yalikuwa ni 'People's Power'






No comments: