SNAKE PARK-ARUSHA.
Wiki hii Mpini Wa Shoka na familia waliamua kujimwaga kidogo kwenye bustani ya wanyama, eneo la duka bovu, Barabara kuu ya Arusha-Dodoma. Wakati mwingine ukijihisi kichwa kimebanwa sana na mambo ya hii dunia usiyoweza kamwe kushindana nayo, basi tafuta nafasi utembelee maeneo kama haya. Hapa ni Meserani, ni kilometa chache tu kutoka katikati ya jiji la Arusha. Wengi wanapafahamu zaidi kama Snake Park. Kuna vivutio na vituko viiiiiiiingi; wakina bundi, kenge, nyani, na wengineo wengi wapo. Achilia mbali bustani na vijiji vya asili. Kwa hakika panavutia. Hebu tupia jicho kidogo; huu ni uhondo mchache tu na familia.....
Majoka ya kila aina yakiwa yamewekewa vioo kwa ajili ya kutazamwa.
Anko Saadi Abdillahi yeye akaamua apate pozi kidogo kwenye uzio wa mamba.
Bwana mkubwa Saidi Mustafa na mdogo wake Faidha Mustafa nao hawakucheza mbali
Kuna msemo unaosema "mtoto wa nyoka ni nyoka". Basi hawa ni watoto wa mamba, nao ni.......
Picha ya juu wanaowachungulia watoto hawa wa mamba ndani ya bwawa lao, kutoka kushoto ni Khadija Saidi Kivuyo na mjukuu wake, Sumaiyah Jigge, katikati ni mama Saadi pamoja na anti yake, Shadya Jigge mwenye kilemba cheupe anayechungulia kwa woga; na Khadija Abdallah 'Mama Shadya'.
Hii ni aina ya mamba mweusi. Huyu ni balaa tupu
Kanga wamepozi kwa raha zao.
Picha ya pamoja ya familia pembeni mwa Ngamia. Wengine wanaogopa ile mbaya. Ni presha juu.
Bibi na mjukuu wake; Khadija Saidi Kivuyo na Sumaiyah Jigge
Khadija Abdallah na wanawe; Sumaiyah aliyebebwa, Shadya mwenye kilemba cheupe anayeonekana wazi amejawa na woga juu ya Ngamia waliyesimama pembeni mwake. NA aliyevaa shati la njano ni Anko Saadi Abdillahi.
Mambo ya juu kwa juu. Hidaya, Ashura na Renata wakiendesha Ngamia.
Mtu na shemeji yake; ni mwendo mdundo.
Kumbe unaweza hata ukalala kabisa usingizi na kupiga kajimluzi tartiiiiiiibu! Lakini chunga usalama wako. Ni bora uanguke wewe, kuliko huyo mtoto aliyekaa katikati. Mambo ya Meserani haya....
No comments:
Post a Comment