SOWETO-ARUSHA

Soweto mjini Arusha ni eneo maarufu lenye nyumba za AICC-Arusha International Conference Centre. Ni nyumba za miaka mingi mno. Wapo waliozaliwa, wakalelewa na kukulia ndani ya nyumba hizi kwa miaka mingi (miaka nenda rudi). Kwa sasa nyumba hizi zipo katika mchakato wa kuvunjwa. Inawezekana AICC wanao mpango kamambe wa kujenga nyumba nyingine mpya za kisasa katika eneo hili. Baadhi ya nyumba hizo kongwe tayari zimekwishaanza kupigwa 'rungu' kama unavyojionea mwenyewe hapo chini. Hapa ni upande wa barabara ya Florida.


Hii tayari imekwishalazwa chini! Na hiyo iliyobaki kwa mbele nayo iko mbioni.






Kwa mbali unajionea 'kitu' kimeinuliwa. Ni miongoni mwa maghorofa yanayochomoza kwa kasi hivi sasa kila upande wa mji wa Arusha. Ni jengo jipya kabisa linaloelekea kukamilika.


 

Barabara ya Florida inaonekana kwa mbele


No comments: