UFUGAJI-KUKU
"Ukipenda boga, basi upende na ua lake" Ni msemo maarufu. Wengi wetu tunaipenda sana nyama ya kuku, lakini kuwafuga kuku na kuwapa matunzo sahihi yanayotakiwa huwa ni kazi ngumu mno. Tunapenda kufuga kuku kwa mtindo "wa akajitafutie mwenyewe mchana kutwa" na jioni ajirudie ndani ya kibanda alale. Lakini akitaga yai tunashangilia kwa nguvu kwamba ni yai letu na kujisifu kwamba sisi ndio tunaomfuga kuku huyu. Aaah, wapi wewe! Ni uonevu na unyonyaji tu huo. Matunzo mazuri ya kuku huanzia wakati wanapokuwa bado ni vifaranga wadogo kama hawa unaowaona hapa. Watunzwe mahali salama, hasa kwa ulinzi wao dhidi ya wanyama na ndege hatari kama vile vipanga, vicheche na mwewe. Wapewe chakula cha kushiba na maji safi. Wewe mwenyewe utafurahia jinsi wanavyokuwa vizuri. Hapo sasa na wewe ndipo utajigamba kwamba kweli unafuga. Siyo wajifuge wenyewe, na wewe kazi yako iwe ni kuyashangilia tu mayai yanapotagwa!
No comments:
Post a Comment