KIJIWENI!
Kwa haraka tu akili inaweza ikakutuma kwamba hawa wote wanafahamiana vema, na wako pamoja. Lakini ukiyatuliza vizuri macho yako, ni dhahiri utagundua kila mmojawao hapa huenda hamjui yeyote yule kati ya hawa aliokaa nao. Yawezekana kila mtu ana mambo yake yasiyohusiana kabisa na yeyote yule hapa. Ndivyo mambo ya vijiweni wakati mwingine huwa hivyo. Watu wanakaa pamoja kama hivi wanavyoonekana hawa, eneo la kwa Mromboo-Arusha, lakini kumbe hata hawajuani kabisa. Mambo ya mishemishe za mjini!
No comments:
Post a Comment