MAMBO YA UBUNIFU HAYA.

Huu ni mchoro tu kwenye karatasi. Utundu na ubunifu wowote ule mzuri hutegemea zaidi kichwa na akili ya yule anayejaribu kuifanya kazi hiyo. Atachora! Na kisha tena mara atafuta hapa... atarekebisha pale. Na baada ya kuridhishwa na mchoro wake, ambao wakati wote huenda na vipimo, ndipo sasa ataianza rasmi kazi ya kukitengeneza kwa vitendo kile kilichopo kwenye mchora wa karatasi yake. Hili ni dirisha lenye mchanganyiko wa mbao na vyuma (nondo). Kazi ni kwako mbunifu.

No comments: