BAADA YA USHINDI....

    Siku ya Jumamosi ya Tarehe 10/11/2012, Diwani mpya wa kata ya Daraja Mbili mjini Arusha Mheshimiwa Prosper Remmy Msoffe atakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara na wananchi wote wa kata ya Daraja Mbili, utakaofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Daraja Mbili kuanzia majira ya saa nane ya mchana.

     Huu utakuwa ndio mkutano wa kwanza kabisa kwa Diwani Prosper Remmy Msoffe kuzungumza na wananchi wa kata yake, tangu alipofanikiwa kuchaguliwa katika uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi uliofanyika tarehe 28/10/2012, kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo, marehemu Bashir Msangi. 

     Mheshimiwa Prosper Remmy Msoffe aligombea katika uchaguzi huo kupitia bendera ya 'People's Power' Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini-Chadema, na kufanikiwa kuwashinda wagombea wengine kupitia vyama vya CCM, CUF, NCCR-mageuzi na TLP.    

     Haya, kazi ni kwako mwana-Daraja Mbili ukamsikilize diwani wako anasema nini juu ya kata yako.




Hii ilikuwa ni siku moja tu baada ya kutangazwa msindi wa nafasi ya kiti cha udiwani. Akipongezwa na kusalimiana.

No comments: