MITI NI UHAI...MITI NI KIVUTIO CHA MAZINGIRA.
Ingawa kuna juhudi kubwa kubwa tu kote duniani za kuhimizana juu ya upandaji, ukuzaji na uangalizi wa kutosha wa miti na misitu kwa faida ya dunia yenyewe na viumbe vyake vyote vilivyo hai, na hasa binadamu na wanyama, lakini pia ni vema kuitunza miti ili iweze kuvutia na kupendeza na hasa ile iliyopandwa majumbani, badala ya kuiacha ijikuze ovyo tu hata kufikia hatua ya kuwa ni yenye kutisha na kuchukiza.
Bwana mkubwa huyu na panga lake mkononi nilimfuma mjini Arusha akiifanyia usafi baadhi ya miti, kwa kuiondolea matawi yasiyofaa ili iendelee kupendeza na kuvutia zaidi kwa kila mtu.
Na wewe je, nyumbani ama shambani kwako miti inavutia au inatisha?
Pigo moja tu, tawi lisilotakiwa chini! Bwana mkubwa amejipinda kisawasawa na panga lake mkononi kwa mkono wa kushoto. NI kazi tu kwa kwenda mbele...
Rundo chini la matawi yasiyotakiwa yaliyopunguzwa mtini
No comments:
Post a Comment