MAJENGO-ARUSHA

Lori likipasua katika mmojawapo wa mitaa ya eneo la Majengo ya juu. Sijui hata limebeba nini hili! Hapa katika mtaa huu, ndugu yangu usiombe mvua ipige. Utapapenda mwenyewe kwa hilo tope la kukata na shoka. Vigari vidogovidogo vya kutembelea huwa vinakiona cha mtema kuni. Sina uhakika sana kama wakati wa zoezi tamu linaloendelea katika Mji wa Arusha la kuziwekea lami barabara za katikati ya Mji linalofanywa kwa ufanisi mkubwa na wa-China ( picha hapo chini) litaweza kuzifikia barabara za mitaa kama huu, ambayo mingine imegeuzwa hata ndiyo mahali pa kutupia taka na kumwaga maji machafu kwa wakazi wa mitaa hiyo! Jiji siyo eneo la katikati tu mwa mji; hata maeneo ya pembeni kwa akina kajamba nani nayo yanatakiwa yapewe uangalizi na matengenezo yanayostahili kwa sababu nao pia ni wakazi wa Jiji.

 

No comments: