UTOTO, BWANA! RAHA TUPU.

 Ninapomtazama binti yangu huyu mdogo wakati wote anapojitahidi kujifunza kutembea kwa ufasaha, huku mara kadhaa akipiga mieleka akipinduka ovyo kama gari, huwa nacheka sana. "eti hata mimi baba yake naye pia nilikuwa hivi!" "Na hata mama yake naye pia alikuwa vivi hivi!" Ama, kweli maisha ya mwanadamu hapa duniani ni kichekesho kitupu. Ndipo huwa narudi kuyakumbuka maneno fulani ya Mwenyeezi Mungu katika maandiko ambayo yanabainisha waziwazi hekima na uwezo wake mkuu, kwamba yeye huvileta viumbe katika hali ya udhaifu, na kisha huvipa nguvu na maarifa; na kisha huvirejesha katika hali ya udhaifu na kuviondolea nguvu zote. Kuletwa katika hali ya udhaifu ni kama hivi kibinti hiki kisivyoweza kujimudu kwa sasa katika harakati zake za kutembea vema, lakini baadaye huyu atakuwa mkubwa na kuwa na nguvu na maarifa mengi tu. Lakini tena atarejeshwa katika udhaifu uleule wa utotoni akifikia uzeeni! 


Na pipi kijiti mkononi tunajaribu kupiga hatua.




 Tunasimama kidogo tunaangalia huku na kule kama mashabiki wapo, na wanatuangalia ili watupongeze japo kidogo.




Tunajaribu kupanda kwenye sehemu hii ngumu na pipi kijiti yetu mkononi hatuiachi japo inagusa chini kwenye mchanga, ili kuonesha uwezo wetu.



Si unaona mwenyewe nimeweza! Haya naingia kwenye banda la kuku kuwaona kuku wa bibi yangu. Na wewe unataka kuja? Karibu.

No comments: