KITU KIPYA KINAUNDWA HAPA!
BodaBoda hiyo na safari zake. Huenda jamaa anajaribu kumuwahi kwa mbele huyo mteja aliyejipigilia mwilini suti ya nguvu. Hapa ni katika eneo maarufu Mjini Arusha ambalo linatazamana kabisa na ofisi za kikosi cha Zimamoto-maeneo ya Faya (Fire). Kuna kitu Wa-china wameamua kukiunda hapa. Panatengenezwa mzunguko wa magari (keepleft) kwa ajili ya barabara ya Fire inayotokea hoteli ya New Arusha na barabara mpya iliyochongwa ambayo inatayarishwa kuwekwa lami siku siyo nyingi sana ambayo inaanzia kwenye mzunguko (keepleft) uliopo jirani na viwanja vya NMC (Soko jipya) na kwenda kutokea Njiro kwa kupitia kwenye daraja jipya linalojengwa mto Themi (nyuma ya nyumba za polisi) hadi barabara mpya ilichongwa pembezoni mwa mlima Shabaha (Themi Hill). Aisee, mbona patapendesa sana, msee wangu! Hebu kodoa visuri macho yako hapa chini.
No comments:
Post a Comment