BARIADI.

...lakini wakati nikiendelea kurandaranda kwa raha zote katika Mji huu wa Bariadi, ghafla tu siku chache kabla ya kuondoka kurejea mjini Musoma-Mara, Bi mkubwa wangu (mama) akapatwa na hali ya kuugua ghafla tu! Huenda ni hali ya hewa na maji ndivyo vilivyomkorofisha mwilini. Niliingiwa na mshituko mwingi, lakini kwa hakika Mwenyezi Mungu alimtunza.....   

Hapa akiwa ameuchapa kabisa usingizi mzito, baada ya hali yake kuanza kutulia na kumpa unafuu wa maumivu ya mwili. Alitundikiwa drip 4 za maji na madonge kibao!


Hii ndiyo Zahanati ambayo Bi mkubwa wangu alilazwa. Nawashukuru sana manesi na madaktari wa Zahanati hii kwa huduma yao. Inaitwa Mwana Leguma Dispensary-Bariadi; Simiyu. 

 

No comments: