SERA ZA MGOMBEA WAKO!
Siku moja kabla sijauacha rasmi Mji wa Bariadi, mara nikagongana na mwanasiasa huyu. Pamoja na mambo kadhaa niliyoongea naye, lakini maandalizi yake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Tanzania kwa mwaka 2015 yamekwishaanza rasmi. Ameshaanza kujiandaa vilivyo kwa ajili ya kutaka kumwangusha diwani aliyepo sasa katika kata yake iliyopo Bariadi mjini, ili yeye ndiye akikalie kiti hicho. Yeye ni Mgombea kupitia Chama Cha Mheshimiwa John Momose Cheyo cha United Democrat Party-U.D.P.
Na hiki ni mojawapo ya vipeperushi vyake vya maandalizi kwa ajili ya uchaguzi huo wa mwaka 2015.
Wakwetu, hebu jisomee kwa makini wewe mwenyewe ujionee. Usije ukasema nahodha wako wa Mpini Wa Shoka nimeongezea chumvi na asali zaidi.....
....na kilichonivutia zaidi katika kipeperushi hiki, ni uwepo wa picha ya mwanamuziki wa kimarekani wa miondoko ya kufokafoka, 50 Cent! Sasa sijui ndiye mfadhili wake katika uchaguzi huo wa 2015 au vipi!
Hii ndiyo sura ya pozi la mgombea wako, sura ya kazi tayari kwa mapambano ya udiwani katika kata ya Malambo, Bariadi mjini mwaka 2015. Wakwetu, upo! Na wewe umekwishaanza kujiandaa, au umebaki kukalia porojo tupu tu za mitaani!
No comments:
Post a Comment