MPINI WA SHOKA UNAKUPA MKONO WA 2013. PAMOJA SANA.

Kwa hakika, nakushukuru kwa kuniunga mkono kwa kupita ndani ya www.mpiniwashoka.blogspot.com kwa mwaka 2012. Nakuomba uupokee mkono wangu wa 2013. Lakini nakukumbusha tu kwamba, kuingia kwa mwaka mpya hakumaanishi chochote kile kwako endapo hautojitahidi kujituma zaidi. Upya wa mwaka ni namba tu, Wakwetu; hakukubadilishii chochote kile cha maana. Lakini Upya wa hatua yako fulani utakayoipiga kwa mwaka huu wa 2013 ambayo haukuwa nayo kamwe, au hata kwa miaka mingi sana umeshindwa kabisa kuifikia, huo ndio upya utakaokuwa wa maana zaidi kwako, na kwa maisha yako yote. Na tumkumbuke sana yule aliyetuumba kwa udongo, ambaye ni lazima kwake siku fulani tusiyoijua tutarejea tu mbele zake kwa njia ya kifo, njia ambayo nyoyo zetu wengi kwa hakika hatuipendi kabisa....

Haka kabinti kangu kadogo kalining'ang'ania kwelikweli siku hii ndani ya gari hili, ili na kenyewe nako kakupe mkono wa 2013 pamoja na mimi. Anaitwa Sumaiyah. Machachari hako! Wee wacha tu! Kizazi cha digital hiki! Happy New Year!

 

No comments: