HIVI NDIVYO JUMANNE TAREHE 01/01/2013 ILIVYOONEKANA KWENYE KARIBU MITAA YOTE YA KATIKATI YA MJI WA ARUSHA.
Kwa kawaida, hizi ambazo Mpini Wa Shoka ulijaribu kuzipitia, ni zile ambazo kwa siku za kawaida huwa na msongamano mkubwa wa watu na magari....
Picha hizi mbili kwenye barabara ya Makongoro inayopita makao makuu ya Polisi hadi kwenye mnara wa Azimio la Arusha na kutokea ubavuni mwa uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid. Ni nyeupe kabisa
Hizi nazo ni kwenye barabara inayotoka stendi kuu ya mabasi ikipitia Golden Rose hadi Mianzini. Nayo ilikuwa ni nyeupe kabisa.
Hapa ni kwenye stendi kubwa ya usafiri wa ndani ya Mji-stendi ya daladala
Hapakuwa na msongamano wowote ule uliozoeleka wa magari na watu. Magari yalikuwa ni machache mno, na hata abiria pia.
Sehemu za foleni za daladala ndizo hazikuwa na magari kabisa.
Karibu vibanda na maduka yote ya biashara katika stendi hii ya usafiri wa daladala vilikuwa vimefungwa.
Ni maeneo ya msikiti mkuu wa Arusha (uliofichwafichwa kidogo na miti upande wa kulia), jirani na Mnara wa Azimio la Arusha. Ghorofa jeupe kushoto unaloliona linaitwa Sinkcourt hotel, ambalo inafahamika zaidi mjini Arusha kama jengo la Sunda. Chini kidogo ya Ghorofa hili utakutana na hospitali ya St. Thomas ya Tanzania. Sijui kama hospitali hii ina uhusiano wowote ule na ile ya London nchini Uingereza alikofia mwalimu Julius K. Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania! Barabara hii maarufu nayo ilikuwa ni nyeupe kabisa kama unavyoiona.
STENDI BINAFSI YA MABASI!
Hii ni barabara iliyowekwa lami hivi karibuni tu. Ipo ubavuni na stendi ya mabasi ambayo hayapakizi wala kushusha abiria wake kwenye stendi kubwa iliyopo katikati ya Mji. Stendi hii ipo jirani kabisa na stendi kubwa ya daladala. Mengi ya mabasi hapa ni yale yanayokwenda Dar es salaam, Musoma na hata Morogoro. Inafahamika zaidi na wengi kama stendi ya Dar express. Ni kwa wale abiria ambao hawapendi kero za stendi kubwa za nauli zisizoeleweka pamoja na bughudha za wapiga debe na wakatisha tiketi wasiokuwa na mpangilio. Barabara hii nayo haikuwa na msongamano wowote ule wa watu na magari. Jengo la rangi ya pinki isiyokolea sana linaloonekana kulia, ni hospitali kubwa inayofahamika kwa jina la Seliani.
No comments:
Post a Comment