BAADA YA KITCHEN PARTY ARUSHA; HATIMAYE NDOA IKATIMIZWA RASMI...



Baada jioni ya siku ya Alhamisi ya Tarehe 20/06/2013 kwenye ukumbi wa Shule ya Msingi Uhuru, katikati ya Jiji la Arusha, kufanywa sherehe ndogo ya kumuaga rasmi, hatimaye ndoa kamili ya mdogo wetu Amina Hemedi Charema wa mtaa wa Jamhuri-Arusha imefanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 22/06/2013 kwa mafanikio makubwa nyumbani kwao na baba zake, huko mtaa wa Ibaya-Kijiji cha Shighatini-Kata ya Shighatini Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. Mpini Wa Shoka nao ulifanikiwa kupanda hadi juu kabisa ya vilele vya milima mikali kuelekea Shighatini na kufika mtaa wa Ibaya kuishuhudia shughuli hii....

 

 

Upande wa Bwana Harusi ukiingia rasmi nyumbani kwa Bibi Harusi kwa mbwembwe, nderemo na vifijo wakilizungusha hewani kila upande begi lililojaa vifaa chungu nzima walivyomletea Bibi Harusi wao.

 

Bwana Harusi na wapambe wake wakiwasili nyumbani kwao Bibi Harusi tayari kwa ajili ya kufungishwa ndoa... 




Wamekaa chini kwa utulivu baada ya kukaribishwa na wenyeji wao. Bwana Harusi ni Ramadhani Yasini Msemo (katikati) akiwa na wasindikizaji wake...




Hapa ndipo penye shughuli yenyewe. Bwana Ramadhani Yasini Msemo akifungishwa ndoa mbele ya mashuhuda na mashahidi, ukiwemo Mpini Wa Shoka




Baada ya kufungishwa ndoa, Bwana Harusi Ramadhani Yasini Msemo akaweka uthibitisho wake kwa kusaini hati (cheti) ya ndoa mbele ya mashahidi na mashuhuda




Kama weye una wivu...!




Bibi Harusi, Amina Hemedi Charema, naye 'akimwaga' uthibitisho wake kwa kuweka saini kwamba ni kweli ameolewa na Bwana Ramadhani Yasini Msemo, huku bwana harusi akishuhudia pembeni mwake. Yaani ni raha tupu! Wee, acha tu!



 

Miserebuko ya kila aina kabla na baada ya ndoa. Yaani, ilikuwa ni raha tupu ndani ya mtaa wa Ibaya-kijiji cha Shighatini. Na ngoma za asili na vionjo vya kidini ndivyo hasa vilivyotawala muda wote... Watu wote: watoto kwa wazee, Wazee kwa vijana, walijiachia vilivyo kwa raha zao...


Baba mkubwa wa Bibi Harusi, Selemani Charema (mwenye tai) pamoja na babu wa Bibi Harusi, Mzee Quraish Mfinanga (mwenye miwani kulia) nao pia hawakuacha kuonesha hisia zao za furaha kwa miserebuko ya hapa na pale, huku wakiwa wamezungukwa na ndugu, jamaa, majirani na marafiki kutoka pande mbalimbali  




Shangazi wa Bibi Harusi, Yasmini Charema 'mama Aisha' akimkamata mkono mdogo wa Bibi Harusi, Ahmedi Hemedi, ili wanaswe vizuri na kamera ya Mpini Wa Shoka wakati wa miserebuko..





Bibi wa Bibi Harusi, bibi Amina Hemedi Mfinanga, anaonekana akiwa amesafiri mbali mno kimawazo huku mkono ukiwa kiunoni. Usiwaze sana bibi; wajina wako atakwenda kuishi salama tu huko aendako na mumewe..




Wengine walibaki wameduwaa tu. Haieleweki ni kwa furaha au ni kwa sababu ya kitu gani hasa..! Swahiba, fundi Husseini Mndorwe (katikati) naye anatazama kwa makini vijimambo vinavyoendelea shughulini





Kutoka kushoto (mwenye shati jeupe) ni Mzee Walii Charema, Hemedi Charema (baba mzazi wa Bibi Harusi), Mzee Nuhu Mfinanga na Babu Mzee Manara




Baba wadogo wa Bibi Harusi. Picha ya Juu mwenye shati jeupe ni Sekizenji Nuhu 'Seki'. Picha ya chini: aliyesimama ni Hemedi na aliyekaa ni dereva Juma Nuhu 




Mambo ya 'mibonyezo' (chakula) yalikuwa ya kutosha. Wenye 'nafasi' zao za kutosha matumboni 'walijipigilia' vilivyo




Mdogo wa Bibi Harusi, Rashidi Hemedi (aliyenyoosha mkono) akiwa maeneo ya matayarisho ya 'msosi' (chakula) pamoja na baba zake wadogo na nduguze wengine. Hapa anaukaribisha Mpini Wa Shoka usogee jirani kwenye masuala mazima ya 'kubonyeza' msosi. Mpini Wa Shoka haukujivunga..Sahani moja kubwa iliyoshehenezwa vema ndizi mshale kwa nyama za kutosha ikasogezwa karibu; kazi ikaanza.... 





Kwenye nyumba hii ndipo hasa shughuli hii nzima ya kufungisha ndoa pamoja na sherehe za harusi ilipofanyika




 

Mdogo wa Bibi Harusi, Tatu Hemedi Charema, naye pia alikuwepo, akiwa 'amejipigilia' vazi la nguvu. Jamani! Eti, amependeza au hajapendeza?




Angalia kwa makini katikati ya umati huu utamwona Bibi Harusi, Amina Hemedi Charema, amefunikwa shela kichwani. Hapa ndipo msafara wa kumpeleka nyumbani kwao na mumewe ulipoanza. Ni nyimbo, vigeregere, shangwe, nderemo, hoihoi na vifijo vitupu vya kila aina. Mambo ni kiasili na kidini tu hapa Shighatini wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro. 


No comments: