TUWAKUMBUKE WAPENDWA WETU WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI, KWA KUYATEMBELEA MAKABURI YAO, KUYASAFISHA NA KUWAOMBEA DUA NJEMA; KISHA NA TUZIKUMBUSHE SANA NAFSI ZETU WAKATI WOTE KWAMBA, IKO SIKU ISIYOKUWA NA JINA NA SISI PIA TULIOBAKI HAI TUTALAZWA NDANI YA ARDHI KAMA WAO TULIVYOTANGULIA KUWALAZA…


Bibi Fatuma Mohammed Laizer 'Mama Hassani' aliyesafiri kwa gari kutoka nyumbani kwake, Majengo-Arusha, akilifanyia usafi mojawapo ya makaburi ya ndugu, jamaa pamoja na watoto zake waliolazwa katika makaburi ya familia yaliyopo Ngaramtoni ya chini, nje kidogo ya Jiji la Arusha.





Hapa akiwa na ndugu yake, Babu Abdillahi Mohammed Laizer wa Simanjiro-Manyara, wakijadiliana jambo fulani huku wakiendelea na kazi ya usafi wa makaburi





Wakifanya dua na maombi ya pamoja baada ya kumaliza kazi ya usafi





Mmoja wa watoto wa Bibi Fatuma Mohammed Laizer 'Mama Hassani', Anko Mohammed Salim Soloka wa Majengo-Arusha (kushoto), naye pia alikuwepo katika ziara hii. Kulia ni kiongozi wa Msikiti wa Ngaramtoni ya chini (unaoonekana kwa nyuma) aliyeongoza shughuli hii.



No comments: