SAFU ZA VILIMA VYA WILAYA YA MWANGA-KILIMANJARO

 

Unapobahatika kufika katika Mji wa Mwanga uliopo pembezoni mwa barabara Kuu ya Arusha-Moshi-Tanga-Dar es Salaam, basi usipumbazike na sura ya Mji huo. Ukitaka kuifaidi vema wilaya hii ambayo ni nyumbani kwa Waziri wa zamani wa Fedha wa enzi za Mwalimu Nyerere, Mzee Cleopa David Msuya, na pia kwa mmoja wa mawaziri wa Serikali ya sasa ya JK (Jakaya Kikwete), Mheshimiwa Jumanne Maghembe, basi ifuate barabara ya lami iliyopo katika Mji huu inayopanda juu kwenye vilima virefu vyenye kona kali za hatari, ambazo kama dereva wa gari lenu atakuwa ni mwenye roho nyepesi, yawezekana kabisa akashindwa kuendelea na safari na akagoma kabisa kupanda juu zaidi... 



Mpini Wa Shoka ukiwa juu kabisa ya mojawapo ya vilele vya vilima hivi, katika Kata ya Shighatini




Tazama kwa makini katikati ya msitu utaziona barabara zilivyogawanyika huku na kule. Mojawapo ya barabara hizi, ndiyo ambayo Mpini Wa Shoka uliitumia hadi kufika juu kabisa 



Juu ya vilele vya vilima unayaona makazi (nyumba) za wenyeji (wakazi), ambao kwa asili ni wa jamii za kabila la Wapare. Barabara za kuyafikia makazi haya zinaonekana vema, ambapo wenyeji wenyewe ndio wanaochukua jukumu la kujitengenezea (kuchonga) wenyewe 



Mpini Wa Shoka ukiwa juu kabisa katika Kata hii ya Shighatini, ukafanikiwa kuliona kwa mbali Ziwa Jipe, ambalo kwa eneo hili ndilo mpaka wa nchi za Tanzania na Kenya. Juu ya vilele vya vilima hivi, pia Bwawa maarufu kwa uvuvi wa samaki (Bwawa la nyumba ya Mungu) nalo pia huwa linaonekana vema kabisa




Mapori na vichaka vikubwa kwa vidogo vilivyostawi vema juu ya vilele vya vilima





Mashamba ya mazao ya aina mbalimbali, hasa ndizi na miwa



Nyumba za wenyeji (wakazi)




Nyumba ikiwa imezingirwa na migomba ya ndizi iliyostawi vilivyo kwenye mwinuko mkali




Mojawapo ya barabara za kuelekea kwenye makazi (nyumba) ya wenyeji, ambazo wamejitengenezea wenyewe...




Wakati ukirejea chini ukitokea huko juu ya vilele vya vilima, hivi ndivyo Mji wa Mwanga unavyoanza kuonekana kwa mbali... Na wewe pia jaribu wakati fulani upate fursa ya kuvitembelea vilele vya vilima hivi vya wilaya hii ya Mwanga

No comments: