KIJIJI CHA UJAMAA-OLJORO ARUSHA



HIVI NDIVYO KINAVYOONEKANA KWA NYAKATI ZA JIONI. Mpini Wa Shoka ULIPITA HAPA GHAFLA TU NA UZURURAJI WAKE WAKATI WA JIONI MOJA (JUA LIKIELEKEA KUZAMA). KWENYE PICHA HII, HAPA NDIPO ENEO LA MJINI (CENTER au MADUKANI). NI KIJIJI KILICHOPO KWENYE BARABARA KUU YA ARUSHA-SIMANJIRO-KITETO; MWENDO WA KAMA 40Km na kitu hivi, KUTOKA ARUSHA MJINI...



Hii ndio taswira ya maisha halisi ya makazi ya wananchi wengi wa vijijini... Hata katika kijiji hiki, napo pia wapo watu maarufu na wataalamu mbalimbali waliozaliwa, kusomea na hata kukulia katika kijiji kama hiki, ambao kwa sasa wakiwa wametawanyika kila mahali katika nchi na hata dunia nzima kwa ujumla; lakini je, leo watu hao wanakumbuka kupatembelea japo hata kwa mara chachechache tu ili kujaribu kuziinua nguvu na bidii za maendeleo, na hasa kwa yale mambo magumu ambayo hata wao waliwahi kuyapitia wakati walipokuwa wadogo ndani ya kijiji hiki, hasa upatikanaji wa maji safi na elimu?

No comments: