NI AJALI, LAKINI NI KITUKO!


Mpini Wa Shoka ulikutana na tukio hili wakati nikiwa nimesafiri binafsi tu kutoka Arusha mjini kwenda Mji (kijiji) wa M'buyuni uliopo wastani wa kilometa 38 hadi 39 kutoka katikati ya Mji wa Arusha kwa kupitia barabara Kuu ya Arusha-Simanjiri- Kiteto. Ni ajali ya aina yake, ingawa hapakuwepo na mtu hata mmoja aliyedhurika kwa namna yoyote ile. Stori yenyewe iko hivi: Lori la rangi ya kijani, aina ya Scania likiwa limesheni mchanga kutoka machimbo ya mchanga ya Mirongoine (tazama machimbo ya Mirongoine kwenye picha za chini), lilijikuta likishindwa kukipanda kilima maarufu kilichopo eneo la CCM (mwendo wa kama km 6 au 7 hivi kutoka Arusha mjini), na ndipo dereva wake akaamua alibinulie pembezoni mwa barabara. Sasa siku iliyofuata, lori la rangi nyekundu aina ya Fiat nalo lilipokuwa likikipanda kilima hiki na mchanga likajikuta likishindwa. Katika harakati za kujiokoa, ndipo dereva wa gari hili akajikuta amelivamia lori la rangi ya kijana; yote mawili yakabaki yamekwama....!


Jamaa kwenye picha ndiye aliyeachwa na wenzake wa lori la rangi nyekundu, ili alinde usalama, ndiye aliyenisimulia mkasa huu wa aina yake. Ni kama vile ni filamu fulani hivi ya kusisimua! 




Unaziona 'ngoma' jinsi zilivyoumana?

No comments: