FRIENDS CORNER-ARUSHA


       Mataa ya kuongozea magari (Traffic lights), Friends Corner




Hapa ni kwenye kituo cha mafuta cha BP-Friends Corner (siku hizi kinaitwa Puma) Upande anakoelekea yule mama mwenye gauni la rangi nyeupe kidogo, ni mwelekeo wa kwenda viwanja vya N.M.C (siku hizi soko jipya), hadi pande za maeneo ya Ungalimited na Sokoni One




Mataa ya kuongozea magari (Traffic lights) yanavyoonekana vema. Jengo jeupe kushoto ni benki ya C.R.D.B (Co-operative and Rular Development Bank)  tawi la Friends Corner




Pikipiki na LandRover ya wazi zimesimama kwenye mataa zikisubiri kuruhusiwa. Wote wanatokea mwelekeo wa viwanja vya N.M.C (siku hizi soko jipya), pamoja na pande za Ungalimited na Sokoni One. Kwa mbele; upande ule linakoelekea gari dogo la rangi nyeupe, ni mwelekeo wa kwenda Stendi Kuu ya mabasi pamoja na Soko Kuu la Arusha  


No comments: