LA HAULA! MBONA NI KAMA KWENYE SINEMA VILE!


Pande Za Sinoni...

Ni wakati wa usiku; karibu sasa 4 hivi, Mpini Wa Shoka na dogo Rashidi Hemedi Charema 'Shidi' wakitokea kwenye mizunguko yao ya hapa na pale, mara ghafla wakakutana na kihoja hiki! Unaweza usiamini kamwe, lakini hivi ndivyo ilivyotokea. Dereva mwanamume aliyejipigilia suti ya maana aliyekuwa akiliendesha gari hili alijikuta akishindwa kulimiliki kwenye kona kali iliyopo Maeneo ya Sinoni jirani na nyumba za askari-polisi (jirani kabisa na duka la muhindi), na kujikuta badala ya kunyoosha usukani kwenye lami, kona aliyoikata ikamzamisha kwenye ukuta huu. Dereva alitoka salama, ingawa alionekana wazi alikuwa amelewa chakari... 




Dogo Rashidi Hemedi Charema 'Shidi', akitabasamu wakati tulipokuwa tukiishangaa ajali hii ya aina yake. Pembeni yake ni mwanadada ambaye naye alifika hapa kushuhudia. Sikuweza kulipata jina lake...





Kitu hadi ndani! Lakini swali la Mpini Wa Shoka ni hili, mjenzi wa ukuta huu aliujenga kwa viwango vinavyotakiwa, na hasa aina ya matofali aliyoyatumia! Au ni uchakachuzi tu kama kawaida...!



  

 

 Kwa Mromboo nako...

Fid Fosi. Ni maeneo ya jirani kabisa na kambi ya askari wa F.F.U (Field Force Unity); mwendo mfupi tu kufika kwa Mromboo. Mpini Wa Shoka ukalishuhudia gari hili dogo likiwa limerushwa pembeni. Hapa pia mwendo ulimshinda dereva, ndipo mambo yakawa kama hivi unavyojionea. Hakuna aliyedhurika. Lori pembeni linajaribu kutoa msaada wa kulivuta kutoka mtaroni...

No comments: