HILI LINAFAA KUWA KAPU LA SADAKA NDANI YA NYUMBA YAKO YA IBADA? AU LIONGEZWE KIDOGO UKUBWA!


Nje ya lango Kuu la kuingilia ndani ya Kiwanda cha Bia Arusha (Breweries) Themi Hill, kila siku Mpini Wa Shoka unapopita mahali hapa huwa unamkuta mzee huyu akiwa amesimama kwa mtindo huuhuu, na mavazi hayahaya akilishona kapu hili! Sijui kama analiuza, au kila anapomaliza kulitengeneza moja, analipeleka nyumbani kisha anaanza tena kutengeneza jingine jipya ambalo linafanana kabisa na hili! Lakini ndani ya tolori la mbao ambalo kapu limewekwa juu yake, mzee huyu anauza bidhaa ndogondogo kama pipi na sigara...







Hii ni barabara inayopita nje ya lango Kuu la kuingilia ndani ya Kiwanda cha Bia Arusha (Breweries), ambako mzee mtengeneza kapu anapatikana. Ukuta wote unaoonekana ni wa kiwanda cha Bia. Wachina pia wapo kwenye barabara hii wakiifanyia mambo mazuri kama mwenyewe unavyoiona ilivyotulia kwa lami mupya. Tazama kwa makini mkono wa kulia, ni mwinuko wa kilima cha Themi (Themi Hill)  

No comments: