MTAA WA NDOVU-ARUSHA

 

Ni mtaa uliopo katikati ya Mji. Ni jirani na Stendi Kuu ya Mabasi na pia ni jirani sana na Soko Kuu. Kwa wenyeji wa Mji wa Arusha, sifa kubwa ya mtaa huu ni biashara ya uuzaji wa mchele...



Barabara ya mtaa huu ni miongoni mwa barabara chache za Mji wa Arusha ambazo lami yake haikuwa imechakaa sana kwa kuharibika. Lakini hata hivyo, katika mpango wa maboresho ya Mji wa Arusha, barabara hii nayo pia imelambishwa lami muuuupya! Si unajionea mwenyewe? Mbele kabisa mwa picha hii unaonekana kwa mbali ukuta wa Soko Kuu (wenye mlango mweupe wa duka)




Hapa ni kwenye makutano ya kwenda Msikiti wa Bondeni (kwa Shehe Shabani) hadi maeneo ya stendi Kuu ya mabasi (upande huo anakoelekea mama mwenye gauni la rangi nyekundu.) Nyuma ya gari kulia ni barabara ya kwenda msikiti Mkuu wa Arusha na shule ya Sekondari ya Bondeni. Ukipanda na upande huo wanakoonekana watu wengi wakitembea, ni jirani kabisa na Uwanja wa Michezo wa Sheikh Amri Abeid pamoja na jengo la ofisi za CCM-Mkoa. Unaliona hili ghorofa kushoto kwako linavyopanda kwenye mtaa huu?  

No comments: