CHADEMA NDICHO KIDUME CHA JIJI LA ARUSHA CHAGUZI NDOGO ZA NAFASI ZA UDIWANI...! CHAJIZOLEA KWA KISHINDO KATA ZOTE...


CHAGUZI HIZO zilifanyika siku ya Jumapili tarehe 14/07/2013. Kata zilizofanya chaguzi za Madiwani wake, ni pamoja na Elerai, Themi, Kaloleni na Kimandolu. Uchaguzi huo mdogo ulifanyika ili kuziba nafasi za madiwani waliokuwepo kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kutimuliwa na chama chao. Pamoja na kuwepo kwa vyama kadhaa vilivyosimamisha wagombea katika chaguzi hizo ndogo, na kampeni kuchukua nafasi yake, lakini maono ya wazi kabisa yalionesha kuwa vyama vitatu vya CCM, CHADEMA na CUF, ndivyo ambavyo vingekuwa katika ushindani mkubwa. Na hivyo ndivyo ilivyotokea; lakini CHADEMA ndicho kilichofanya kweli zaidi katika chaguzi hizo, baada ya kuvigaragaza vilivyo vyama vyote vilivyoshiriki katika chaguzi hizo kwa kushinda kwa kishindo katika kata zote...   

Peopleeeeeeeeeeeeeees Power..! 

 

 

 Furaha ya wana-CHADEMA haikuwa pekee tu kwa wale wa zile Kata ambazo wameshinda katika chaguzi hizi ndogo. Hata wapenzi na wanachama wa chama hicho katika mitaa, vitongoji na Kata nyingine zote za Jiji la Arusha nao pia walikuwa ndani ya furaha kubwa ya kuusherehekea ushindi huo mtamu kwa kufanikiwa kuzirejesha mikononi mwao Kata zao walizokuwa wameshinda katika uchaguzi mkuu uliopita. Katika pitapita zake, Mpini Wa Shoka uligongana na wakereketwa pamoja na wafurukutwa wa chama hicho katika Kata ya Daraja Mbili, kwenye kijiwe cha Madereva Teksi wa Sinoni kilichopo kwenye kituo kipya cha kuoshea magari (CarWash) cha Sinoni-Mwsho wa lami kiitwacho 'A' Town CarWash. Aliyepeperusha angani vidole vya ushindi ni dereva Antoni, na mwenye shati la rangi nyeupe aliyeoneshea vidole kwa pembeni ni Dereva Mussa Kijiko.  



No comments: