KAZI NI ILEILE, LAKINI NI KATIKA MAENEO TOFAUTI! NA NI KATIKA VYOMBO VIWILI TOFAUTI...

 

Hapa ni kwenye viunga vya mitaa ya Majengo...

 

Wanamume wanapambana vilivyo kuisaka noti kwa udi na uvumba. Mkokoteni umeshibishwa vilivyo mzigo. Ubavuni umeandikwa 'KIKULACHO' NO.1'




"Aisee vipi! Hapo nyuma mbona hamsukumi? Mnategea!"




Haya, twende kwa pamoja....oooop!




 

Hapa ni Sinoni-Daraja Mbili...

 

Hawa wenyewe wana kagari kao. Hapa hakuna habari ya kusukuma wala kutegeana. Ni Sinoni-Daraja Mbili; maeneo ya jirani na bwawa la Maji machafu (majitaka). Gari la kukusanya vyuma chakavu (scrapers) linajiandaa kutumbukia ndani ya maji ya mto (mbele kidogo tu ya huyo mwendesha baiskeli kulia), ambapo ndipo ilipo chemba kubwa inayoyaunganisha mabomba yote ya maji machafu (majitaka) katika Jiji la Arusha, na kuyapeleka kwenye bwawa la maji machafu (majitaka) ambalo lipo jirani kabisa na mahali hapa.

No comments: