JUU YA MLIMA THEMI (MLIMA SHABAHA)-ARUSHA, NAPO PIA WACHINA WAMEFANYA VITU VYAO VYA UHAKIKA...


Hii ni miongoni mwa barabara mpya kabisa zilizochongwa miaka ya hivi majuzi tu ndani ya Jiji la Arusha na kuwekewa lami na wachina. Ni Barabara inayopita juu-pembezoni mwa Mlima Themi (Mlima Shabaha), ikiunganishwa na barabara inayotokea kiwanda cha Bia-Themi na kupita eneo la viwanda (Kiltex na Tanzania Litho-Leathor); kisha inakwenda kutokea eneo la Relini (jirani na kiwanda cha matairi-General Tyre). Ni ka-barabara katamu kwelikweli...



Mpini Wa Shoka ukiyashuhudia magari makubwa kwa madogo yakiwa juu mlimani. Hapa yanaelekea upande wa eneo la viwanda (Kiltex na Tanzania Leathor hadi kiwanda cha bia-Themi). Lakini pia unaweza ukapenyapenya kwa njia za ndani kwa ndani hadi maeneo ya Daraja Mbili, Sinoni hadi Unga Limited kwa kutumia barabara za vumbi.. 

 

 

Na hapa unateremka kwa mwendo wa kasi kutokea juu ya mlima na kwenda moja kwa moja hadi eneo la Relini (jirani na kiwanda cha matairi-General Tyre) hadi Njiro. Mmoja wa wafanyakazi wa ujenzi wa barabara, anaonekana vema kulia akiwa kazini na mashine ndogo ya kushindilia pembezoni mwa barabara... 

No comments: