LINAONEKANA NI KAMA BWAWA ZURI LA KUVUTIA LA MRADI WA UFUGAJI WA SAMAKI...! LAKINI KUMBE...


Mpini Wa Shoka ukiwa umesimama kwenye barabara mpya ya lami iliyotengenezwa hivi karibuni kwa juu kwenye kilima cha Themi (Shabaha), ukawa unaliona vema bwawa hili maridadi; bwawa la kuvutia kwelikweli. Kwa mtu mgeni asiyelifahamu vema bwawa hili anaweza akahisi hata ni bwawa la kufugia samaki, lakini kumbe wapi! Hili ndilo bwawa kuu la kuhifadhi majitaka (maji machafu+vinyesi) ya wakazi na wananchi wote wa Jiji la Arusha. Majitaka haya huwa yanafikishwa katika bwawa hili kwa njia mbili kuu. Njia ya kwanza ni ile ya magari ya majitaka yanayokwenda kuvuta bidhaa hiyo huku na kule kwenye majumba ya watu. Na njia ya pili ni ile ya mabomba ya moja kwa moja ya majitaka yaliyounganishwa kwenye majengo kadhaa ya makazi na ya biashara, ingawa njia hii bado imebaki kuwa ni kwa baadhi tu ya wananchi wachache, kwani asilima kubwa ya wananchi wa Jiji la Arusha na vitongoji vyake hawana huduma hii...       

No comments: