MAZOEA YAKIZIDI SANA KWENYE KAZI ULIYOIZOEA, MATOKEO YAKE HATA SEHEMU ZA HATARI UNAWEZA UKAJIKUTA UKIZIFANYIA MZAHA KWA USALAMA WAKO MWENYEWE...!


Mpini Wa Shoka ulimfuma swahiba huyu akiwa juu ya jengo la mojawapo ya vituo cha kuoshea magari (CarWash) kwenye mtaa wa Jamhuri-Kata ya Daraja Mbili jijini Arusha akiwa na mwenzake wakifanya shughuli yao ya ufundi kwenye tenki la maji...

Hebu tazama jinsi anavyouweka rehani usalama wake kwa sababu ya mazoea tu ya kazi yake..!



Jina lake Maarufu anaitwa Kibakuli. Hapa anamrushia kipande cha bomba mwenzake aliyeko chini ya jengo..





Kisha, anaanza kushuka chini kwa kutumia mabomba ya maji huku miguuni akiwa hana hata kandambili (malapa) tu, achilia mbali viatu vya kazi...! 






Baada ya kufanikiwa kuteremka kwa kutumia mabomba, anaambaambaa pembezoni mwa kibaraza cha jengo huku akiuonesha Mpini Wa Shoka jinsi yeye alivyo hodari na imara katika kuuchezea usalama wake kazini..! 






Mwenzake aliyebaki chini, fundi Kitaringo, akimsubiri bila ya hofu wala wasiwasi wowote ule ili ashuke waendelee na kazi nyingine..!

No comments: