URAFIKI MWINGINE NI BALAA TUPU!



Anaitwa Sumaiyah Jigge. Ni binti yangu mdogo. Hivi karibuni nilipokwenda kuwasalimia nyumbani kwa bibi yao maeneo ya Njiro-Arusha, alinipokea kwa kunitaka nimpokee zawadi ya kumbeba Paka huyu! Kwa hakika, Binti yangu huyu mdogo na Paka huyu wamezoeana kupita kiasi. Ukiwakuta wakati wanapokuwa wakicheza pamoja kwa namna ambayo Paka huyu anakuwa amejilegeza kabisa kama vile hana ukali wowote ule wa makucha yake, utabaki unashangaa tu! Ama kweli, urafiki mwingine ni balaa tupu! 

No comments: