BURUDANI KWA WATOTO; IMEWASOGELEA JIRANI KABISA. HAKUNA SABABU YA KWENDA MBALI SAAAAAAANA NA MAKAZI YAO....


Ni burudani iliyoanzishwa hivi karibuni, kwenye mtaa wa Jamhuri ndani ya Kata ya Daraja Mbili kwenye viwanja vya kituo cha kuoshea magari cha Jamhuri (Jamhuri Carwash), Jijini Arusha. 

Katika pitapita zake, Mpini Wa Shoka ulifika katika eneo hili na kujionea jinsi watoto wanavyojilia starehe na burudani kwa raha zao....


Wakiwa wamekaa tayari, kabla bembea halijaanza kuzunguka



 

Mabosi wakiwa juu ya farasi weupe wakisubiri mzunguko uanze





Hawa wao siyo kwamba wana mikia ya rangi ya bluu; hapana. Nao pia wamekaa juu ya farasi wa rangi ya bluu tayari kwa mzunguko..





Mmilikiwa wa kituo cha kuoshea magari cha Jamhuri (Jamhuri Carwash), Bw. Joseph Shirima, maarufu zaidi kwa jina la Matokeo a.k.a Mwanangu, (mwenye fimbo mkononi-kulia) ambaye pia ndiye mmiliki wa burudani hii ya watoto, akiwa na mmoja wa wazazi waliofika kuwashuhudia watoto wakiburudika kwenye michezo mbalimbali....





Hawa wao juu ya farasi wa rangi ya njano...Lakini mbona ninyi warembo mmenuna namna hii? Au mnaogopa!





Haya! Mzunguko umeanza. Kila mmoja ajikamate vema....





Binti wa mmiliki wa burudani hii, Marry Shirima 'Marry G' (kulia) akijadiliana jambo fulani na mmoja wa vijana wa mtaa wa Jamhuri, Iddi Jumanne 'Mwamba' wakati watoto walipokuwa wakiendelea na michezo yao... 

 

"...kama vipi, na wewe weekend moja bebana na watoto wako, muje muje; baje baburudike weeeeeeeee hadi benyewe bachoke na nyoyo zao"


No comments: