VYOVYOTE VILE ULIVYOSHEREHEKEA; Mpini Wa Shoka UNAKUPA MKONO WA IDDI


Waislamu pande mbalimbali za Arusha, waliungana na waislamu wengine kote duniani katika kuisherehekea Sikukuu ya Idd El Fitri, baada ya kuikamilisha safari ya masiku machache tu (29 au 30) ya kuufunga (saumu) mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Baada ya sala ya Idd mapema asubuhi kwenye viwanja vya wazi na ndani ya misikiti, nyuso za tabasamu na furaha ndizo zilizotawala kila upande....







Kukumbatiana kwa bashasha na mahaba kama hivi, ndiko kulikotawala zaidi





Na kama kawaida, waheshimiwa wadogowadogo kama hawa iliwabidi wawe wakipatiwa msaada wa kuvalishwa viatu. Vinginevyo, uvaaji wao ulikuwa ni wa vihoja vitupu; kulia-kushoto, kushoto-kulia!





Furaha na raha nyusoni kwa akina mama pia havikufichika hata kidogo 





Khadija Saidi Tilya (mwenye mtandio wa rangi ya zambarau) na Khadija Abdallah Chembe (aliyebeba mtoto), wakitoka msikitini kwenye sala ya Idd pamoja na waumini wengine. Anayewafuata nyuma ni Bi. Ashura.



Akbar Ally (mwenye kofia ya rangi nyeupe) na Rashid Omary katika pozi la picha ya Sikukuu ya Idd, kwenye msikiti uliopo eneo la Tanesco-Njiro





Hapa ni Ramadhani Abdallah, Swalehe Rashid na Rashid Omary

 

 EID MUBARAK



No comments: